Recent Posts

Wednesday, August 15, 2012

MADEE ASEMA BADO NI MSHABIKI MKUBWA WA DOGO JANJA.

Madee
Aliyekuwa manager wa Dogo Janja ,Rapper Madee amesema bado yeye ni mshabiki mkubwa wa Dogo Janja na anaikubali sana ngoma mpya ya Dogo Janja inayoitwa Ya moyoni.Madee amesema anaujua Uwezo wa dogo janja na hii ngoma aliofanya imeonyesha wazi Dogo anaweza kufanya Ngoma tofauti inayohusu maisha .Hii ngoma itamsogeza anapotaka yeye . Kilicho mvutia Madee ni chorus ambayo amesema ina Feeling nzuri na PNC amefanya powa ingawa ningeiskia kabla ya kwenda Radio basi kuna marekebisha madogo ningempa PNC ila sikupata nafasi hio, Pia Marco Chali amefanya yake kwa kumpa beat nzuri na hizo ndio beat za Dogo Janja . Kuhusu idea ya wimbo mimi nimeipenda na ilikuwa kwenye wazo langu baada ya ngoma yake na chegge angetoa ngoma kama hio inayo ongelea maisha yake . Kuhusu Madee kuongelewa kwenye ngoma hio ,Madee amesema hajaskia kitu chochote kinacho muhusu kwenye hio Ngoma na anavyo elewa Ya Moyoni ni mambo yako binafsi na nitofauti na ya Mdomoni ambayo nikama unamsema mtu .Kila mtu ana Yamoyoni so ipo siku na mimi nitasema ya moyoni

0 comments:

Post a Comment